20 Mar 2023 / 125 views
Ratiba ya mechi za FA

Manchester City itamenyana na Sheffield United katika nusu fainali ya Kombe la FA, huku Brighton ikicheza na Manchester United.

City ilifuzu hadi nne bora kwa ushindi wa 6-0 dhidi ya Burnley Jumamosi.

The Blades iliishinda Blackburn 3-2 Jumapili kabla ya Brighton kumaliza ndoto ya Ligi ya Pili ya Grimsby kutinga hatua ya nane bora kwa ushindi wa 5-0.

Katika robo fainali iliyopita, Manchester United ilitoka nyuma na kuichapa Fulham 3-1 katika uwanja wa Old Trafford. Nusu fainali zote mbili zitafanyika kwenye Uwanja wa Wembley wikendi ya 22-23 Aprili.

Mshambuliaji nyota wa City Erling Haaland alifunga hat-trick yake ya pili ndani ya siku tano katika ushindi huo dhidi ya Clarets.

Hii itakuwa nusu fainali ya kwanza ya Sheffield United ya Kombe la FA tangu 2014.

Wachezaji waliokopwa hawaruhusiwi kucheza dhidi ya vilabu wazazi katika Kombe la FA, kumaanisha kuwa wenzi wa Blades Tommy Doyle na Jamie McAtee hawataruhusiwa kucheza dhidi ya washindi mara sita wa shindano hilo City.

Doyle alifunga bao la kufutia machozi dakika za lala salama dhidi ya Blackburn na kuwapeleka Blades Wembley.

Brighton walifika nusu fainali ya Kombe la FA mara ya mwisho mwaka 2019 huku Manchester United wakiwa washindi mara 12.